NJIA RAHISI YA KUTANGAZA BIASHARA YAKO:

Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia matangazo (marketing) inabeba nafasi kubwa sana katika kufanya biashara imfikie mlaji kiurahisi na hivyo kuleta maendeleo katika biashara. Biashara za kukaa na kusubiri wateja waje zimepitwa na wakati, inatakiwa ubuni mbinu za kuwafuata wateja walipo. Nimeandika baadhi ya njia za kutangaza biashara, jaribu kuzifuata utaona matokeo.

1) Tengeneza vipeperushi na business cards, zisambaze kwa kila mtu unayeona anafaa kuwa mteja wako.
2)Tumia mitandao ya kijamii kujitangaza kama Facebook, Instagram
3)Tumia vyombo vya habari kama radio, televisheni na magazeti
4)Andaa matamasha utakayotumia kujitangaza
5)Hudhuria matamasha mbalimbali yaliyoandaliwa na utumie kujitangaza.
5)Tumia magari ya matangazo kutangaza huduma au bidhaa zako
6)Kuwa na utaratibu wa kuwa na siku ya punguzo la bei (promotion day)
7)Toa huduma iliyobora wateja wataletana wenyewe. (Good customer care)
8)Ajiri watu kwa ajili ya kutangaza bidhaa zako na unawalipa kutokana na wateja aliwaleta. Unawalipa kwa commision. Na hawa ndio mara nyingi wana nafasi kubwa sana ya kuleta wateja wengi.

Naandaa kitabu kinachohusu biashara, kitaongelea mambo mengi Kutangaza biashara ni mojawapo. Tembelea blog hii mara kwa mara ili kupata taarifa zaidi.

"Mafanikio ni mapambano yasiyohitaji watu wepesi wa kukata tamaa"
DAVID MCHOMVU
Mhamasishaji na Mtoa ushauri kuhusu biashara
Mawasiliano: 0675975251
Email: dmchomvu6@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

JIFUNZE NIDHAMU YA KUWEKA AKIBA YA FEDHA

PATRICK NGOWI SUCESS STORY

HOW ALIKO DANGOTE MADE HIS MONEY