JIFUNZE NIDHAMU YA KUWEKA AKIBA YA FEDHA
KUWEKA AKIBA KUNAHITAJI NIDHAMU Kama unapenda kufanikiwa katika biashara basi anza kujifunza kuwa na nidhamu ya matumizi bora ya fedha unazozipata. Inawezekana umeajiriwa na unapata mshahara kila mwisho wa mwezi, Je kuna kiasi chochote cha pesa huwa unabakisha kama akiba? Maisha hayatabiriki kuna mambo mengi mbele yetu ambayo kwa namna yeyote ile hatuwezi kuyatabiri (unforeseen events) akiba imekuwa mkombozi mkubwa kwa matatizo ya aina hiyo. Kama unapenda kuanza biashara na huna kabisa mtaji wa kuanza nao ila una mahali unapata hela kama malipo, basi nakushauri anza kuwa na mipango thabiti ya kuweka akiba. Jiwekee wajibu ambao ni lazima uutimize kila siku, unaweza kujiwekea wajibu wa kuweka 500 kila siku. Hii itakusaidia sana kuwa na nidhamu ya fedha lakini pia kujibana kwa ajili ya kitu fulani. Najua watu wengi wamekuwa na matamanio ya kuweka akiba lakini huwa wanashindwa njiani na kuitumia akiba waliyoweka eti kwa sababu walikuwa na uhitaji wa fedha kwa wakati huo hivyo wakaona...