KWA NINI BIASHARA YAKO HAIFANIKIWI
1)Ni mwepesi wa kukata tamaa, unahisi biashara ndio imeshakufa na huna haja ya kujipanga tena kuiimarisha. Changamoto ndogo unashindwa kukabiliana nazo unakuwa mwepesi wa kuacha changamoto zikutawale badala ya kupambana nazo uzishinde.
2)Sio Mbunifu, Unashindwa kuwa mbunifu katika biashara unayoifanya na kufanya wateja wako waone hauna jipya. Tangu umefungua biashara yako hujawahi kufanya jambo lolote la utofauti ili kuongeza thamani na kuwavutia wateja. Wateja wameshachoka kuona kitu unachokiuza kila siku unatakiwa kuweka ubunifu ili kuongeza thamani na kufanya biashara yako kuwa mpya machoni kwa watu.
3)Hujaelewa wateja wako wanataka nini zaidi, unatumia nguvu nyingi, pesa na muda kufanya kile ambacho kinakupendeza wewe machoni na sio kinachowapendeza wateja. Kama bado hujalingundua hilo rudi sokoni chunguza wateja wanataka nini sio wewe unapenda nini. Cheza na soko linataka nini kwa wakati gani.
4)Huwajali wafanyakazi wako, huwapi huduma zinazostahili na hivyo hawaoni kama na wao ni part ya biashara yako. Unawachukulia kawaida na kuwajali tu katika mishahara. Sikiliza shida za wafanyakazi wako na jaribu kutatua pale inapowezekana, pokea mawazo yao kuhusu biashara uone watakavyojisikia furaha na kufanya kazi kwa kujituma. Kumbuka wao ndio injini kwenye biashara yako, wangekuwa hawana umuhimu usingewaajiri.
5)Huipendi biashara unayoifanya, jiulize hiyo biashara ndio biashara ya ndoto zako? unamapenzi nayo au unaifanya tu kwa sababu rafiki zako walikushawishi. Kama huipendi basi hutumii nguvu na muda mwingi kuifanya isimame. Fanya biashara unayoipenda zaidi utaona matokeo.
6) Hauna kumbukumbu za mapato na matumizi hivyo huelewi mwelekeo wa biashara yako, ukiwa na shida ya hela wewe unachota tu kwa sababu biashara ni yako, unajikuta unatumia hela nyingi za nje ili kuongeza mtaji wakati biashara inatakiwa ikuzalishie na ijiongeze yenyewe. Kumbukumbu ni muhimu sana. Nunua daftari andika kila kitu kinachohusu hela inayotoka kwenye biashara utaona matokeo.
Imeandaliwa na:-
DAVID MCHOMVU
Mhamasishaji na Mshauri wa Biashara
Simu: 0675975251
Email: dmchomvu6@gmail.com

Comments
Post a Comment